Tanzania

Baadhi  ya vijana Tanzania bado wanashindwa kuhusisha SDGs na maisha yao- Hussein Melele

Vijana wengi nchini Tanzania wanaelewa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini si wengi wanaofahamu ni kwa namna gani malengo hayo yaliyopitishwa mwaka 2015 yanayahusiana moja kwa moja maisha yao.

Sauti -
3'48"

Taasisi ya Benjamin Mkapa yasaidia kuimarisha huduma za afya vijijini kwa kuwandaa wahudumu wa afya

Miongoni mwa taasisi hizo ni ile ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania ambayo kwa kushirikiana na serikali ina miradi mbali mbali ya kuhakikisha wakazi wa vijini wanapata huduma ya afya na watoa huduma nao wanavutiwa kufanya kazi maeneo hayo kama anavyofafanua Dkt Ellen Mkondya Senkoro, Afisa Mtendaj

Sauti -
2'39"

Taasisi ya Benjamin Mkapa yasaidia kuimarisha huduma za afya vijijini- Dkt. Ellen

Taasisi za kiraia zimeendelea kushirikiana na serikali hususan katika nchi zinazoendelea ili kuweka mazingira bora ya kazi maeneo ya vijijini kwa wahudumu wa afya na hivyo kufanikisha lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu kuhusu afya bora na ustawi kwa wote.

Vituo vyetu vya msaada wa sheria huanzishwa kwa kuzingatia mahitaij yaliyopo- WLAC

Nchini Tanzania kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, WLAC kimekuwa msaada hasa kwenye maeneo ambako bado kuna changamoto kuhusu haki na sheria.

Sauti -
4'15"

Kukomesha usafirishaji haramu ni jukumu la dunia nzima:UN

Usafirishaji haramu wa binadamu ni uhalifu mbaya kabisa na unagusa kila pembe ya dunia, huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake, wasichana na watoto umesema leo Umoja wa Mataifa. Arnold Kayanda na ripoti kamili. 

Sauti -
3'55"

30 Julai 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Janga la usafirishaji haramu wa binadamu ni la dunia nzima likiathiri zaidi wanawake, wasichana na watoto umesema Umoja wa Mataifa ukitaka hatua zaidi zichukuliwe kuukomesha

Sauti -
15'6"

Usafirishaji haramu wa binadamu ni dondandugu la kila nchi-UN

Usafirishaji haramu wa binadamu ni uhalifu mbaya kabisa na unagusa kila pembe ya dunia, huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake, wasichana na watoto umesema leo Umoja wa Mataifa.

29 Julai 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea 

Sauti -
13'23"

Iwapo ulizikosa wiki hii ya 22-26 Julai 2019

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA, Yukia Amano, aaga dunia, siku chache tu kabla ya kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu wadhifa huo. Suala la wahamiaji na wakimbizi wanaosaka maisha bora barani Ulaya kupitia Mediteranea lapigiwa chepuo kwa hatua mpya chanya barani humo. Nchini Kenya mradi mpya kwenye pwani ya nchi hiyo washamirisha mikoko na biashara ya hewa ya ukaa. Baa la nzige latishia mustakabali wa chakula kwenye pembe ya Afrika na Yemen, na mtoto Mwigulu ambaye alikatwa mkono kisa tu ni albino azungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.

Licha ya kupungua kwa mashambulio dhidi ya watu wenye ualbino, wanaishi kwa mashaka na hofu

Ingawa vitendo vya watu wenye nia ya uovu wa kuwashambulia watu wenye ualbino kuonekana kupungua, bado watu wenye ualbino wanaishi kwa mashaka na hofu kutokana na madhila wanayopitia katika maisha yao ya kila siku.

Sauti -
5'30"