Tanzania

Ninapoona wanawake wana amani hiyo inanipa hamasa kuendelea kuwasaidia- Private Deborah

Umoja wa Mataifa  umekuwa kila uchao  ukipaza sauti kuhusu umuhimu wa uwepo wa walinda amani wanawake kwenye vikosi vya ulinzi wa amani vya chombo hicho.

Sauti -
4'

Barani Afrika bado wanawake na wasichana wanakabiliwa na vikwazo lukuki, tubadilike- UNESCO

Ukatili wa kijinsia, uwakilishi mdogo katika uongozi wa tasnia ya habari na kutowezeshwa kujimudu kiuchumi ni moja ya changamoto zinazoendelea kuwakabili wanawake wengi barani Afrika ikiwemo nchini Tanzania.

Sauti -
1'54"

UNESCO imejitoa kimasomaso kuwasaidia wanawake Tanzania:Do Santos 

Ukatili wa kijinsia, uwakilishi mdogo katika uongozi wa tasnia ya habari na kutowezeshwa kujimudu kiuchumi ni moja ya changamoto zinazoendelea kuwakabili wanawake wengi barani Afrika ikiwemo nchini Tanzania. 

Tunalinda amani lakini pia twawajengea uwezo wa kujipatia kipato- Mlinda amani wa Tanzania nchini DRC

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,

Sauti -
2'6"

04 Machi 2019

Habari za wakati huu hii leo tunaanzia na masuala ya hewa chafuzi na jinsi inasababisha vifo vya watu milioni 7 kila mwaka.

Sauti -
11'28"

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania waleta nuru kwa wanawake DRC

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO wamezungumzia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wanayowapatia wanawake nchini humo yamebadili maisha yao.

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa vitendo.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje.

Sauti -
4'53"

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza kwa vitendo lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje. Nchini Tanzania, moja ya mataifa yaliyoridhia malengo hayo, jeshi la wananchi, JWTZ limeitikia wito huo kupitia shule ambazo inazimiliki. Luteni Kanali Semunyu wa JWTZ alishiriki kikao kilichosheheni maofisa wa ngazi mbalimbali za kijeshi pamoja na wale wanaoongoza taasisi za elimu zilizoko chini ya JWTZ.