Tanzania

Kwa miaka mitatu UNA imepata mafanikio makubwa Tanzania:UNA 

Umoja wa Mataifa umekuwa na mchango mkubwa katika kushirikisha umma wa Tanzania kwenye harakati za uchagizaji na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs kupitia mbinu mbalimbali ikiwemo mashirika yake na miradi yake. Miongoni mwa mchagizaji mkubwa wa malengo hayo ni UNA.

Mila na desturi Kilimanjaro bado ni kikwazo cha haki ya mwanamke:Minde

Mila na desturi zimeendelea kuwa mtihani mkumu katika juhudi za ukombozi wa mwanamke katika kupata haki na sheria  sehemu mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, kwa nini? .

Ulinzi wa raia DRC sio usalama tu, lishe na kipato pia:Mlinda amani Liuma

Mara nyingi tunaposikia ulinzi wa amani taswira inayokuja ni kubeba mtutu, kushika doria na hata kuwafurusha waasi, lakini kumbe ni zaidi ya hayo husuasn kwa jamii husika kwa mujibu wa mlinda amani wa Tanzania kutoka kikosi maalumu cha kujibu mashambulizi FIB cha  ujumbe wa  Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO. Flora Nducha anafafanua zaidi.

UNESCO imejitoa kimasomaso kuwasaidia wanawake Tanzania:Do Santos 

Ukatili wa kijinsia, uwakilishi mdogo katika uongozi wa tasnia ya habari na kutowezeshwa kujimudu kiuchumi ni moja ya changamoto zinazoendelea kuwakabili wanawake wengi barani Afrika ikiwemo nchini Tanzania. 

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania waleta nuru kwa wanawake DRC

Walinda amani wanawake kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO wamezungumzia jinsi ambavyo mafunzo ya ujasiriamali wanayowapatia wanawake nchini humo yamebadili maisha yao.

Jeshi la wananchi Tanzania, JWTZ lanuia kutekeleza kwa vitendo lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora, unapigia chepuo elimu ambayo si tu jumuishi bali pia inampatia mnufaika stadi za kumkomboa kimaisha, iwe kwa kupata ajira akiwa ofisini au akiwa kwenye medani za nje. Nchini Tanzania, moja ya mataifa yaliyoridhia malengo hayo, jeshi la wananchi, JWTZ limeitikia wito huo kupitia shule ambazo inazimiliki. Luteni Kanali Semunyu wa JWTZ alishiriki kikao kilichosheheni maofisa wa ngazi mbalimbali za kijeshi pamoja na wale wanaoongoza taasisi za elimu zilizoko chini ya JWTZ.