Tanzania

Wadau mkoani Ruvuma nchini Tanzania na harakati za kusongesha afya ya mtoto

Shirika la afya duniani, WHO, linasema upatikanaji wa huduma ya afya ni changamoto katika mataifa mengi hususan yanayoendelea na hivyo ni muhimu kwa serikali

Sauti -
5'18"

22 Februari 2019

Leo Ijumaa tuna mada kwa kina ikimulika harakati za kufanikisha afya hususan kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu huko mkoani Ruvuma nchini Tanzania mwenyeji wako akiwa John Kabambala wa radio washirika Kids Time FM.

Sauti -
9'59"

Kijana mwanafunzi  Tanzania aanzisha klabu kuwasaidia wanafunzi wasioona wafurahie haki ya elimu 

Leo Februari 20 ni siku ya kimataifa ya haki za kijamii ikibeba kauli mbiu, ukitaka amani na maendeleo fanyia kazi haki za kijamii. Umoja wa Mataifa umesema haki hizi ni muhimu kwa ajili ya kuishi kwa amani na maendeleo.

Sauti -
4'1"

Hali ya kisiasa Burundi yatia matumaini- Kafando

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Burundi, Michel Kafando amesema hali ya kisiasa nchini humo imeanza kutia matumaini wakati huu ambapo taifa hilo linajiandaa kufanya uchaguzi mkuu hapo mwakani.

15 Februari 2019

Katika jarida letu la Habari kwa kina ijumaa ya leo Arnold Kayanda anazungumza na mtayarishaji wa maonesho ya sanaa za asili kutoka barani afrika , Mtanzania Rose Luangisa ambaye hivi karibuni ameshiriki maonesho ya Umoja wa Mataika yaliyofanyika makao Makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani

Sauti -
9'52"

14 Februari 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Arnold Kayanda anakuletea 

Sauti -
12'21"

Wamiliki wa radio wasiwabinye wanahabari ili sote tunufaike na matangazo ya radio- Msikilizaji

Ikiwa leo ni siku ya radio duniani , kauli mbiu ikiwa majadiliano, uvumilivu na amani, mkoani Kagera nchini Tanzania wananchi nao wamepaza sauti kuhusu umuhimu wa njia hiyo adhimu ya mawasiliano na kile ambacho kinapaswa kufanyika ili kuhakikisha taarifa kutoka chombo hicho zina mantiki.

Mada kwa kina: Kala Jeremiah na matumizi ya nyimbo zake kutetea haki za watoto na vijana

Nchini Tanzania wasanii wanatumia mbinu mbalimbali kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutambua kuwa msanii ni kioo cha jamii na hivyo akionacho ndicho ambacho anakiwasilisha kwa jamii yake kwa lengo la kuelimisha au kuburudisha jamii hiyo husika.

Msaada zaidi kwa Tanzania wahitajika ili ihudumie vyema wakimbizi- Grandi

Kamishna Mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa ,UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Tanzania akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwekeza zaidi mikoa ya kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ambayo ni nyumbani kwa wakimbizi 330,000. 

Vijana wasichana na wavulana mkoani Mara wasimama kidete kukabiliana na FGM

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la usawa wa kijinsia, ukipaza sauti hatua zichukuliwe ili kutokomeza kitendo cha ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, mkoani Mara nchini Tanzania tayari hatua zinachukuliwa na zinazaa matunda.

Sauti -
4'10"