Kijana Richard Katuma ni mmoja wa vijana ambao kwa wakati mmoja alikuwa ni mchanigaji wa vipindi vyetu kwenye Idhaa ya Kiswahili ya UN News alipokuwa akifanya kazi na moja ya radio washirika, lakini kama anavyosimulia katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii mabadiliko katika maisha yalim
Ikiwa imesalia takribani miaka kumi kufikia mwaka 2030 ambao umepangwa kuwa ukomo wa utimizaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs ,juhudi kote duniani zinaendelea kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.
Ikiwa imesalia takribani miaka kumi kufikia mwaka 2030 ambao umepangwa kuwa ukomo wa utimizaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs ,juhudi kote duniani zinaendelea kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.
Kutoafikiana kwa mataifa yanayochangia kiasi kikubwa cha hewa ukaa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi au COP25 uliohitimishwa mwishoni mwa wiki, kumezifadhaisha nchi zinazoendelea ikiwemo bara la Afrika ambalo si mchangiaji mkubwa wa hewa ukaa lakini ni muathirika mkubwa wa athari zake.
Hii leo Ijumaa mada kwa kina inapiga kambi huko Geita nchini Tanzania ambako Adelina Ukugani anazungumza na wakili Walta Carlos kuhusu ukatili wa kijinsia.
Miongoni mwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa na Umoja wa Mataifa ni kushirikiana na nchi wanachama katika kulinda, kutunza na kuendeleza ipasavyo vyanzo vya maji wakati huu ambapo matumizi holela ya vyanzo hivyo ni sababu kuu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Hii leo siku ya huduma ya afya kwa wote Umoja wa Mataifa wataka serikali zitimize ahadi ya kuwapatia wananchi wao huduma za afya, huko Uganda wananchi wahoji kulikoni viongozi wakiugua wao waende kutibiwa nje, sisi je?