Watu wenye ulemavu wanastahili kujumuishwa pia:Riziki
Mkutano wa 12 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, CRPD, ukiingia wiki yake ya pili hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, wadau wanaendelea kujadili mikakati mbalimbali ya kuhakikisha ahadi ya kutomwacha yeyote nyuma inatekelezwa.