Syria

Chonde chonde pande kinzani Syria zingatieni haki za raia- Bachelet

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesihi pande kinzani kwenye mzozo nchini Syria ziheshimu sheria za kimataifa pindi zinapoendesha operesheni zao za kijeshi wakati huu ambapo usalama wa raia huko Idlib unazidi kuzorota. 

Sauti -
1'51"

Chonde chonde pande kinzani Syria zingatieni haki za raia- Bachelet

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesihi pande kinzani kwenye mzozo nchini Syria ziheshimu sheria za kimataifa pindi zinapoendesha operesheni zao za kijeshi wakati huu ambapo usalama wa raia huko Idlib unazidi kuzorota. 

Basi la aina yake latoa fursa kwa watoto kuwa watoto

Mjini Beirut, nchini Lebanon, basi la aina yake linarandaranda kwenye mitaa ya mji huo likileta furaha, elimu na matumaini kwa watoto wanaofanya kazi mitaani.

Msafara mkubwa kabisa wa msaada wa kibinadamu wawafikia maelfu Rukban:UN

Umoja wa Mataifa na chama cha msalama mwekundu nchini Syria leo wamekamilisha zoezi la kupeleka misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani zaidi ya 40,000 kwenye kambi ya Cyclone Kusini mwa Syria katika msafara na operesheni ambayo ni kubwa kabisa kuwahi kufanywa na Umoja wa Mataifa nchini humo.

Watoto wenye ulemavu si hoja , mtihani ni kuwahudumia na tiba:Mkimbizi Syria

Mama mkimbizi kutoka Syria mwenye watoto wawili wenye ulemavu anasema kuwa na watoto hao si shida mtihani mkubwa unaomkabili ni kuwahudumia na hasa kuwapatia matibabu. Watoto wake wote wawili wana matatizo ya mtindio wa ubongo sasa anahitaji msaada kuwapeleka nchi nyingine.

Sauti -
1'48"

Mke wangu ni shujaa- Samir Al Sayed, mkimbizi kutoka Syria

Wakimbizi wawili wa Syria Wafika na Taha wameishi muda mrefu wa maisha yao wakiwa ndani, wakihangaika kusogea, kuwasiliana na kuchangamana na watu walio karibu yao. Wazazi wao wakikabiliana na uhaba wa huduma kwa ajili ya watu wenye ulemavu, sasa wanaomba msaada wa kupatiwa makazi katika nchi nyingine duniani ambako watawapa huduma nzuri watoto wao. 

Zaidi ya watoto 30 wapoteza maisha Syria kutoka na ghasia na mazingira magumu

Ghasia, ukimbizi wa ndani na mazingira magumu nchini Syria vimesababisha takribani watoto 32 kufariki dunia tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Filamu "Capernaum" kuhusu wakimbizi na wahamiaji yashindania tuzo za Oscars 2019

Nadine Labaki, mwongoza filamu kutoka Lebanon ambaye filamu yake ya Capernaum imechaguliwa kushindania tuzo ya Oscar kwa mwaka huu wa 2019 katika kipengele cha filamu za lugha ya kigeni, amezungmzia kile kilichomfanya kuandaa filamu hiyo inayohusu madhila yanayokumba mamilioni ya watu duniani katika zama za sasa ikiwemo  ukimbizi na uhamiaji.

WHO inatumia njia ya anga kufikisha vifaa vya matibabu kaskazini-mashariki mwa Syria.

Hii leo Shirika la afya ulimwenguni WHO limesafirisha kwa ndege zaidi ya tani 28 za dawa, vifaa vya matibabu na chanjo kwenda katika jimbo la Al-Hasakeh lililopo kaskazini-mashariki mwa Syria kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya matibabu kwenye eneo hilo.

ILO na kazi zenye staha kwa wakimbizi wa Syria nchini Jordan

Nchini Jordan kituo cha kusajili ajira kimekuwa na manufaa makubwa kwa wakimbizi ambao sasa wanajipatia ajira zenye hadhi na utu na hivyo kuweza kukimu siyo tu maisha yao bali pia ya familia zao.