Syria

Tusikate tamaa mzozo wa Syria- Guterres

Mwaka wa 7 wa mzozo wa Syria umekamilika na sasa mwaka wa 8 umeanza na hakuna nuru ya kumalizika kwa mzozo huo, lakini bado tusikate tamaa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo.

Miaka 7 ya vita Syria ni fedheha kwa jamii ya kimataifa: UNHCR

Kumbukumbu ya miaka 7 tangu kuanza kwa vita vya Syria machi mwaka 2011, ni fedhea kubwa kwa jamii ya kimataifa, wanasiasa, serikali ya nchini hiyo na wote ambao wamekaa bila kutafuta muafaka wa kukukomesha janga hilo kubwa la kibinadamu, asema  Filipo Grandi, kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbi UNHCR.

Hatimae misaada ya kibnadamu imefika Ghouta-WFP

Msaada wa kibinadamu kwa eneo la Ghouta mashariki kiunga cha mji mkuu wa Damascus hatimae umeingia eneo hilo. Hii ni kwa mujibu wa ujumbe wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP kupitia ujumbe wake  wamtandao wa  kijamii wa twitter.

Sauti -
1'30"

05 Machi 2018

Katika jarida la leo tunaanza na Syria ambako hatimaye misaada ya kibinadamu imewasili Ghouta Mashariki. Pia tuanangazia wakimbizi wanaorejea nyumbani kwa hiari kutoka Libya. Sikiliza pia makala kuhusu maendeleo ya mji wa Lagos, Nigeria ambako wananchi wanaambatana kukomesha uchafuzi wa mazingira. 

Sauti -
11'27"

Hatimaye misaada ya kibinadamu yaingia Ghouta

Hatimaye misaada ya kibinadamu imewasili Ghouta Mashariki kiunga cha mji mkuu wa Syria, Damascus ikiwa ni ya kwanza tangu katikati ya mwezi Februari. 

Ulinzi na usalama Ghouta bado mtihani mkubwa:Moumtzis

Mtaratibu wa kikanda wa masuala ya kibinadamu kwa ajili ya mgogoro wa Syria amesema anaendelea kutiwa hofu ya usalama na ulinzi wa mamilioni ya raia nchini Syria, ikiwa ni wiki moja tangu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lipige kura kuunga mkono azimio  nambari 2401, linalotaka usitishaji wa mapigano kwa mwezi mmoja nchini Syria.

Syria ifikishwe mbele ya mahakama ya ICC: Zeid

Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito wa mgogoro wa Syria kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC

Sauti -
2'5"

Syria ifikishwe mbele ya mahakama ya ICC: Zeid

Kamisha mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito wa mgogoro wa Syria kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

01 Machi 2018

Jaridani leo tunaangazia ripoti mya ya bodi ya kimataifa ya kudhibiti mihadarati na umuhimu wa madini ya joto au iodine kwa ukuwaji wa mtoto. Pia tunakuletea makala kuhusu athari za matumizi mabaya na ya kupindukia ya viuavijasumu au antibiotics. 

Sauti -
11'33"

UN haitokata tamaa kamwe Syria:De Mistura

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Steffan de Mistura leo amesema Umoja wa Mataifa asilani hautokata tamaa Syria na utaendelea kusisitiza haja ya usitishaji mapigano kunusuru maisha ya watu.