sudan kusini

UNMISS yasambaza tenki za maji sokoni kudhibiti COVID-19 Juba Sudan Kusini

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, katika kuunga mkono juhudi za kitaifa za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona au COVID-19, wamesambaza tenki za maji katika maeneo ya soko yenye msongamano wa watu mjini Juba. 

Hakuna aliye na kinga dhidi ya COVID-19 Sudan Kusini, tupambane nayo pamoja:UNMISS 

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umesema umedhamiria kulisaidia taifa hilo changa kabisa duniani kupambana na janga la corona au COVID-19 wakati huu likiwa katika harakati za kujikwamua kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenye.

04 Mei 2020

 Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa tutaskia :

-Mwendazake Balozi Augustine Mahiga  na mchango wake katika Umoja wa Mataifa.

-Kwa watu waliofanyakazi kwa karibu na Balozi Mahiga wakati wa uhai wake wanasema alikuwa mfano wa mfano wa kuigwa na wanajivunia sana kumfahamu .

Sauti -
13'17"

UNMISS yakarabati barabara jimboni Upper Nile, Sudan Kusini

Walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS wamekarabati barabara za kuunganisha maeneo ya Bunj na Melut yaliyoko mji wa Malakal jimboni Upper Nile, barabara ambazo ziliharibiwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

UNHCR yaendelea kukimbizana na muda kuzuia kusambaa kwa COVID-19 Sudan Kusini

 Katika eneo la Ajoung Thok, maafisa wa UNHCR wanafanya kazi kwa ukaribu na mashirika menmgine ya msaada wa kibinadamu pamoja na serika

Sauti -
2'15"

01 MEI 2020

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa ikiwa siku ya wafanyakazi tunaangazia habari tofauti.

-Leo ikiwa  ni sikukuu ya wafanyakazi,tutaskia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Sauti -
11'52"

UNHCR yaendelea kukimbizana na muda kuzuia kusambaa kwa COVID-19 Sudan Kusini

 Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wanakimbizana na muda kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona nchini Sudan Kusini, nchi changa barani Afrika ambayo iko katika hatua ya kupona kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vililazimisha mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao. 

29 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

Sauti -
11'40"

Manusura wa ukatili wa kingono Sudan Kusini bado wanaishi na jinamizi:UNMISS

Manusura wa ukatili wa kingono nchini Sudan Kusini wengi wao bado wanaishi na jinamizi hilo wakihaha kupata huduma za msingi za afya na hata kujitenga katika jamii kutokana na unyanyapaa. 

8 Aprili 2020

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)

ASSUMPTA:Ni Jumatano 08 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI

Sauti -
12'13"