Chuja:

Stella Vuzo

Shughuli za ununuzi kwenye duka jijini Dar es Salaam, Tanzania wakati huu ambapo kumeripotiwa kutangazwa kwa visa vya corona nchini humo.
UN News/ Stella Vuzo

Tanzania inavyokabili janga la corona

Ni miezi miwili na zaidi sasa tangu Tanzania itangaze mgonjwa wake wa kwanza wa virusi vya COVID-19.  Tangu tarehe 16 mwezi wa tatu mwaka huu mengi yamejiri nchini Tanzania kufuatia kuzuka kwa janga la ugonjwa huo unaoathiri dunia nzima.

Wanawake nchini Chad wakichuuza mboga kwenye soko lisilo rasmi angalau kupata kipato cha kujikidhi maisha yao.
OCHA/Naomi Frerotte

Elimu si karatasi, ni kuelimika

Makadirio ya shirika la kazi duniani ILO yaliyotolewa mwaka uliopita wa 2017, yalionesha kuwa upatikanaji wa ajira kwa vijana utaendelea kuzorota kwa  mwaka huu wa 2018 ambapo vijana milioni 71.1 sawa na asilimia 13.1 ya vijana wote kote duniani hawatakuwa na ajira. Miongoni mwa vijana hao wasiokuwa na fursa ya kupata ajira rasmi ni Situmai Simba msichana mwenye umri wa miaka 24 aliyeanzisha biashara ya uji, ambao kutokana na ubunifu, anamudu kupambana na hali hii ya ukosefu wa ajira kwa kubuni miradi mipya inayowaajiri wao na wenzao.

22 Agosti 2018

Jaridani leo na Siraj Kalyango anaanzia makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kumbukumbu imefanyika leo ya Kofi Annan ikiongozwa na Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres na mwakilishi wa kudumu wa Ghana kwenye Umoja wa Mataifa. Pia anaangazia mkutano unaonza leo kati ya mashirika ya kiraia na Umoja wa Mataifa, ni vipi kwa pamoja wanaweza kusongesha SDGs. Na huko Honduras, vijana waliorejeshwa nyumbani kutoka Mexico na Marekani wafunguka.

Sauti
11'17"