Kipindi cha miezi minane cha makubaliano mapya ya amani nchini Sudan Kusini, kimeshuhudia mauaji ya zaidi ya raia 100 huko eneo la kati la Equatoria nchini humo huku idadi kama hiyo hiyo ya wasichana na wanawake wakibakwa au kufanyiwa ukatili wa kingono kutokana na mapigano mapya.