Skip to main content

Chuja:

silaha

28 Machi 2022

Jaridani Machi 28, 2022 na Leah Mushi tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika changamoto za maji kwenye makambi ya wakimbizi. Pia tutasikia habari kwa ufupi zikiangazia, silaha za vilipuzi, hali ya watoto nchini Syria na ukiukwaji wa haki nchini Libya.

Sauti
12'54"
UNMISS/Ilya Medvedev

Akibutubia WebSummit Ureno, Guterres ataka silaha zenye uwezo wa kuua binadamu kwa kulenga na kujifyatua, zipigwe marufuku

Maendeleo ya teknolojia za kisasa yana faida na hasara zake kwa maisha ya binadamu hivi sasa kwa hiyo ni lazima kuchukua hatua ili kuhakikisha faida inakuwa kuwa kubwa kuliko hasara.

Amesema hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wakati akihutubia jukwaa la wavuti linalofanyika huko Lisbon, Ureno ambapo amesema licha kwamba teknoloja hizo zinarahisisha kazi kama vile utambulisho wa binadamu , kusambaza mgao wa fedha na hata kubaini maeneo yaliyopimwa bado nyingine zinapaswa kuangaliwa upya.

Sauti
2'44"

Machafuko Tanganyika na Kivu Kusini DRC, yawaweka watoto njia panda: UNICEF

Watu zaidi ya millioni moja , wakiwemo watoto 800,000 wamesambaratishwa  na ghasia za kikabila pamoja na mapigano kati ya vikosi vya serikali,dhidi ya makundi  yenye silaha na makundi ya wanamgambo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yaani DRC.

Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto UNICEF, ambalo linasema  vurugu hizo nyingi ziko katika mikoa ya Kivu Kusini na Tanganyika. UNICEF limekariri kuwa kwa sasa idadi kubwa ya watu dunaini waliokimbia makazi yao kutokana na ghasia inapatikana nchini DRC ambako inafikia watu millioni 1.3.