Siku za UN

Ni wakati wa kuwatambua mabaharia na wahudumu wengine wa meli kama wafanyakazi muhimu:UN

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa viongozi kote duniani kuwatambua mabaharia na wafanyakazi wengine wa melini kuwa ni wafanyakazi muhimu kutokana na mchango wao hasa wakati huu wa janga la corona au COVID-19.

WHO yazindua katiba ya usalama wa wahudumu wa afya 

Ikiwa leo ni siku ya usalama wa wagonjwa duniani, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO limeangazia wahudumu wa afya na wagonjwa wanaowahudumia hasa wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ambalo bado linatikisa maeneo mengi duniani. 

Demokrasia ni chachu ya kila kitu katika jamii:Guterres 

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema demokrasia ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa, ushiriki katika ufanyaji maamuzi na uwajibikaji wa kuchukua hatua hasa wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la corona au COVID-19. 

Watu 9 kati ya 10 wanavuta hewa chafu, ni wakati wa kubadili hilo sasa:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa kushikamana na kuchukua hatua zinazohitajika dhidi ya hewa chafu inayovutwa na watu 9 kati ya 10 kila uchao duniani kote.

COVID-19 imevuruga harakati za kukabiliana na ugaidi- Guterres  

Leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa na manusura wa vitendo vya kigaidi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres katika ujumbe wake amesema janga la COVID-19 linakwamisha harakati za kusaidia manusura wa ugaidi.  

Tunasema asante kwa wahudumu wa kibinadamu kokote waliko katika kuokoa maisha-OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibindamu na masula ya dharura OCHA, imeeleza kuwa janga la virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 limeongeza machungu katika changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo watoa huduma za kibinadamu kote duniani

Wahudumu wa kibinadamu ni mashujaa wanaoweka rehani maisha yao ili kuokoa ya wengine:Guterres

Ikiwa leo ni siku ya huduma za kibinadamu duniani Umoja wa Mataifa umesema unawaenzi wahudumu hao ambao wanakabiliana na changamoto lukuki katika kuokoa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu. 

Tuwawezeshe vijana duniani kote ili wachangie katika hatua za pamoja za kimataifa-Guterres

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya vijana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kuhusu siku hii inayolenga ushiriki wa vijana katika hatua za pamoja za kimataifa, ametoa wito kwa viongozi na watu wazima kote duniani kufanya kila linalowezekana kuwawezesha vijana wa ulimwengu kufurahia maisha ya usalama, utu pia fursa na kuchangia katika hatua za pamoja za kimataifa.  

Mikakati ya kupambana na COVID-19 na kurejea katika hali nzuri, iwahusishe watu wa asili

Dunia ikielekea kuadhimisha siku ya watu wa asili keshokutwa Jumapili Agosti 9, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa njia ya video ameeleza kuwa kuna kila haja ya kutambua haki za watu wa asili na kuwajumuisha katika mapambano dhidi ya COVID-19.

Waathirika wa homa ya ini aina B wamepungua 2019:WHO

Kiwango wa watoto wa chini ya miaka mitano wanaougua homa ya ini aina B kilishuka mwaka 2019 hadi chini ya asilimia 1 kutoka asilimia 5 katika miaka 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.