Siku za UN

COVID-19 kutumbukiza mamilioni zaidi ya watu katika umasikini:Guterres

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la corona au COVID-19 litawatumbukiza mamilioni ya watu zaidi katika janga la umasikini. 

Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike: Fursa ya kuunda ulimwengu bora, mzuri na sawa kwa wasichana kila mahali. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya mtoto wa kike anasema wasichana barubaru, na harakati za ulimwengu za mabadiliko wanazounda, ndio viongozi wapya wa wakati wetu.

Kushughulikia afya ya akili ni muhimu katika kufikia uhakika wa afya kwa wote-Guterres  

Kuelekea siku ya afya ya akili inayoadhimishwa kesho Oktoba 10, huku takwimu zikionesha kuwa takribani watu bilioni 1 duniani kote wanaishi na matatizo ya akili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa siku hii amesema, inabidi hatua zichukuliwe ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora ya afya ya akili kwa wote kwani hivi sasa inaonesha pia kuwa kila sekunde 30 mtu mmoja anajiua kutokana na tatizo hili la afya ya akili.  

COVID-19 inaingilia huduma muhimu za afya ya akili yaonya WHO 

Janga la kimataifa la corona au COVID-19 linaingilia huduma muhimu za afya ya akili katika asilimia 93 ya nchi wanachama wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na kuainisha haja ya haraka ya kuongeza ufadhili, limesema shirika hilo la WHO. 

Makazi kwa wote ndio chachu ya mustakbali bora mijini:UN-HABITAT 

Kuwa makazi bora hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ni suala la uhai na kifo hasa janga la corona likiendelea kusambaa duniani na watu wakitakiwa kusalia majumbani, lakini hatua hiyo haiwezekani hasa kwa wale ambao hawana wanapopaita nyumbani limesema shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT. 

Walimu wako mstari wa mbele kufundisha hata zama za sasa za COVID-19 

Kila mwaka, siku ya walimu duniani inatukumbusha dhima muhimu ya walimu katika kufanikisha elimu jumuishi na bora kwa watu wote. 

Katika kuadimisha siku ya kupinga machafuko hebu tusitishe uhasama:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  amerejea wito wake wa kutaka usitishwaji uhasama duniani kote hii leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga machafuko ambayo mwaka huu inafanyika kukiwa na athari mbaya za kiuchumi na kijamii zilizotokana na janga la corona au COVID-19. 

Tunapoadhimisha siku ya utalii , tuwakumbuke watu wa vijijini:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesihi dunia katika wakati huu wa changamoto kubwa zinazoikabili dunia likiwemo janga la corona au COVID-19 ni muhimu kutowasahau watu wanaoishi vijijini katika ahadi ya maendeleo endelevu au SDGs. 

Dawa za uzazi wa mpango zapaswa kupatikana hata wakati wa COVID-19:UN

Fursa ya upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango ni haki ya binadamu inayolindwa chini ya sheria za kimataifa na nchi ni lazima ziendelee kuhakikisha huduma hiyo inapatikana hata wakati wa janga la corona au COVID-19, wamesema wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. 

Silaha za nyuklia si tishio kwa kizazi hiki tu hata kizazi kijacho:UN 

Umoja wa Mataifa umesema utokomezaji wa silaha za nyuklia ambazo ni za maangamizi sio kwa faifa ya amani na usalama wa kizazi hiki tu bali hata vizazi vijavyo.