Chuja:

Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike

UNHCR/Catherine Wachiaya

Hedhi, ndoa za umri mdogo na kutopatiwa fursa vyatukwamisha, tusikilizeni- Watoto wa kike

Leo ikiwa ni siku ya mtoto wa kike duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imebisha hodi huko mkoani  Morogoro nchini Tanzania ambako watoto wa kike pamoja na mwalimu wao wamepaza sauti zao ili kuhakikisha kuwa kundi hilo haliachwi nyuma kwa visingizio lukuki. Umoja wa Mataifa unasema kuwa ahadi yake ya mwaka 2015 inayokoma mwaka 2030 inataka kila mtu ashirikishwe katika harakati za maendeleo, sasa iweje watoto wa kike waenguliwe?

Sauti
4'28"
Binti Zahra kutoka Uganda, ambaye ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya wasichana kushika hatamu au #GirlsTakeover,alishika nafasi ya Mkurugenzi mtendaji wa UNFPA katika siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.
Picha na UN News/Yasmina Guerda

Wasichana wanauwezo wa kuleta mabadiliko, tuwape fursa:UN

Wasichana wengi duniani wanakabiliwa na vikwazo katika safari yao ya kuelekea utuuzima, huku mimba na ndoa za utotoni zikiwalazimisha mamilioni kuacha shule na kukatisha ndoto zao. Hivyo umewadia wakati wa dunia kuchukua hatua na kuwapa fursa ya maisha bora wasichana hawa. Wito huo umetolewa na mkurugenzi mtendani wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, Dkt.Natalia Kanem katika ujumbe kuhusu siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.