Siku ya chakula duniani

Wananchi waishio mijini washauriwa kula vyakula vya asili

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo duniani, FAO na la mpango wa chakula WFP nchini Tanzania wametumia maadhimisho ya siku ya chakula duniani mwishoni mwa wiki yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro kuwataka wananchi kuondokana na kasumba ya kupenda vyakula kutoka nje ya nchi na badala yake wazalishe na kula vyakula vya asili kama njia mojawapo ya siyo tu kuimarisha lishe bali pia mifumo ya uzalishaji chakula. 

Je chakula ulacho kinalinda afya yako na sayari dunia au ndio kinasambaratisha? 

Leo tarehe 16 mwezi Oktoba ni siku ya chakula duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, anasema siyo siku tu ya kukumbushana umuhimu wa chakula kwa kila mkazi wa dunia, bali ni siku ya kutoa wito wa kufanikisha uhakika wa kila mtu kuwa na chakula. 

Njaa inaongezeka kote duniani wakati wa kuchukua hatua ni sasa:Guterres 

Kuelekea siku ya chakula duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 16, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema siku hii sio tu kumbusho la umuhimu wa chakula kwa kila mtu duniani, bali pia ni woto wa kuchua hatua ili kufikia uhakika wa chakula kote duniani. 

16 Oktoba 2020

Katika kumulika wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutaka uwepo wa mifumo himilivu ya kilimo na inayohakikisha upatikanaji wa chakula tunakwenda nchini Tanzania ambako shirika la chakula na ki

Sauti -
10'43"

FAO na WFP waadhimisha siku ya chakula duniani nchini Libya

Mashirika ya Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo dduniani FAO na la mpango wa chakula WFP wameadhimisha siku ya chakula dunini nchini Libya kwa miradi maalumu ya kuisaidia nchi hiyo kufikia lengo la maendeleo la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030.

16 Oktoba 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Leo ni siku ya chakula duniani Katibu Mkuu anasema haikubaliki kuwepo na njaa wakati dunia inatupa tani bilioni moja za chakula kila mwaka

Sauti -
11'7"

Mavuno ya nafaka yaimarika Uganda, lakini bado kuna changamoto- wakulima

Nchini Uganda hali ya upatikanaji wa chakula  imeonekana kuwa bora zaidi kuliko miaka iliyotangulia kutokana na miradi mbalimbali ikiwemo ule wa serikali wa kutokomeza umaskini kwa kuimarisha sekta ya kilimo. Mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda ametembelea familia moja ili kuweza kuhakikisha kauli hiyo.

Watoto wanadumaa kutokana na njaa, hii haikubaliki- Guterres

Takriban watoto milioni 155 duniani kote wanakabiliwa na utapiamlo hali ambayo huenda ikasababisha wakadumaa maisha yao yote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika siku ya chakula duniani hii leo.