Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Siku ya Amani

Wanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi ya Zanaki jijini Dar es Salaam, Tanzania.
World Bank/Sarah Farhat

UN Tanzania yatoa elimu kwa wanafunzi kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu  “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.”

Sauti
2'30"
Katibu Mkuu wa UN António Guterres akipiga Kengele ya Amani wakati wa hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani  mwaka 2025.
UN Photo/Mark Garten

Kengele ya amani yagongwa UN kuikumbusha dunia wakati wa kuchukua hatua kuidumisha ni sasa: Guterres

Leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani hafla maalum imefanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo kwa kawaida huwa kila mwaka tarehe 21 Septemba. Katibu Mkuu António Guterres katika hafla hiyo ameisihi dunia ambayo imeghubikwa na vita na machafuko kila kona kuwa wakati ni sasa kuchukua hatua na kutimiza ndoto ya amani iliyoanza mwaka 1945 baada ya vita vya pili vya dunia.

Sauti
3'18"

21 SEPTEMBA 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi.

Sauti
12'28"
Valentin Flauraud for Saype

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania washerekea Siku ya Amani mkoani Dodoma

Nchini Tanzania katika kuadhimisha siku ya amani duniani, wadau mbalimbali kwa kushirikiana na ofisi ya Umoja Umoja wa Mataifa nchini humo, wameiadhimisha siku hii kwa kupanda miti katika shule ya sekondari Viwandani iliyoko mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia kuondoa amani katika baadhi ya maeneo duniani.

Sauti
2'38"