18 JULAI 2025
Jaridani leo naangazia hafla ya Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela katika makao makuu ya Umoja wa mataifa na ujumbe wa washindi wa Tozo ya Mandela. Makala tunakwenda nchini Angola na mashinani nchini Kenya, kulikoni?

Mapema kabla ya kushiriki hafla hii ya utoaji wa tuzo katika siku hii ya kimataifa ya Nelson Mandela hapa New York, Kennedy Odede alizungumza na Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.
Mapema kabla ya kushiriki hafla hii ya utoaji wa tuzo katika siku hii ya kimataifa ya Nelson Mandela hapa New York, Kennedy Odede alizungumza na Zipporah Musau wa Umoja wa Mataifa.
Umoja wa Mataifa leo umetangaza kwamba Brenda Reynolds, mfanyakazi wa kijamii kutoka jamii ya watu wa asili ya Saulteaux nchini Canada, na Kennedy Odede, mjasiriamali wa kijamii kutoka Kenya, ndiyo washindi wa Tuzo ya Nelson Rolihlahla Mandela ya mwaka 2025.
Elimu ya mtoto wa kike ni moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Wakati ulimwengu unaadhimisha miaka 30 tangu Azimio la Beijing na Jukwaa la Hatua za Utekelezaji kuwekwa bayana, serikali zimetangaza nia ya kisiasa ya kuheshimu, kudumisha haki, usawa na wanawake na wasichana kuwezeshwa.