Idadi ya watalii duniani ilipanda 2017 na huenda ikaongezeka zaidi :UNWTO
Idadi ya watalii wa kimataifa, wanaowasili katika nchi nyingine, na watu wanaoingia nchi moja kwa siku kwa njia halali iliongezeka mwaka wa 2017 kwa kiwango cha asili mia 7 na na hivyo kufikia watalii Zaidi ya millioni elfu moja na mia tatu.
Hii ni kwa mujibu wa vigezo vipya vya shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii duniani UNWTO. Shirika hilo linabashiri kuwa ongezeko hilo litazidi kuvuma mwaka 2018 kwa kiwango cha asili mia kati ya nne na tano.