UN yapongeza Kenya kwa kutumia sheria ya kimataifa kushtaki watuhumiwa wa uhalifu baada ya uchaguzi mkuu 2017
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Türk ameipongeza serikali ya Kenya kwa kile alichoeleza ni hatua muhimu ya kuelekea uwajibikaji kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Kenya, kufuatia uamuzi wake wa wa kutumia Sheria ya Uhalifu wa Kimataifa kuwafungulia mashitaka maafisa wakuu wa polisi kwa mauaji, ubakaji na utesaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo mwaka 2017. Leah Mushi anataarifa zaidi.