serbia

UNMIK/ Video Capture

Waliokuwa mahasimu Kosovo sasa waungana wafungua duka la nyama na kuimarisha utangamano

Eneo la Kosovo ambalo liligubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe hivi sasa liko katika utangamano na wakazi wake chini ya usaidizi wa kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa wanaendelea kusaka mbinu bora za kuleta maelewano baina ya wakosovo wenye asili ya Albania na wale wenye asili ya Serbia. Hatua thabiti zimechukuliwa na wakazi hao ikiwemo wanawake ambao licha ya kutoka jamii tofauti sasa ni kitu kimoja kwa imani yakwamba wanawake wana dhima kuu katika siyo tu ujenzi wa uchumi bali pia amani pale penye mizozano. Je ni kwa vipi basi, fuatana na Grace Kaneiya katika makala hii.

Sauti
4'13"