Security Council

Kwa hapa na pale

Mwakilishi wa UM huko DRC William Lacy Swing amelaani mauwaji ya mwanasiasa Floribert Chuy Bin Kositi, katibu wa jimbo wa chama cha RCD huko Goma, mji mkuu wa Kivu ya Kaskazini. Bw Swing anasema inaonekana kuna mtindo unaojitokeza ya kuwauwa viongozi wa kisiasa na biashara huko mashariki ya taifa hilo kubwa. Mkuu huyo wa MONUC ametoa mwito kwa wakuu wa DRC kuwatafuta na kuwahumu wahalifu wa kitendo hicho cha kikatili kinacho tokea wakati juhudi zina imarishwa kuleta amani katika eneo hilo.

Utekelezaji wa mafikiano na AU juu ya huduma za amani wahitajia kusawazishwa, yakiri Baraza la Usalama

Baraza la Usalama lilipata fursa ya kusikiliza ripoti juu ya matokeo ya ziara ya karibuni ya Tume yake maalumu ambayo ilitembelea Afrika, na ambayo iliongozwa shirika na Balozi Dumisani Kumalo wa Afrika Kusini pamoja na Balozi Emyr Jones-Parry wa Uingereza.

Tume ya Baraza la Usalama imemaliza ziara ya wiki moja Afrika

Wajumbe 15 wanachama wa Tume ya Baraza la Usalama waliozuru mataifa matano ya Afrika kwa wiki moja walikamilisha ziara yao Ijumatano, tarehe 20 Juni katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) anbapo walifanya mazungumzo na watumishi wa UM waliopo huko pamoja na kuonana kwa mashauriano na Raisi Joseph Kabila na maofisa kadha wa Serekali.

Suala la Usomali lazingatiwa tena na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao cha faragha tarehe 14 Juni kusailia hali, kwa ujumla, katika Usomali na pia kusikiliza ripoti ya Lynn Pascoe, Makamu KM juu ya Masuala ya Kisiasa juu ya matukio ya ziara yake ya Usomali hivi majuzi ambapo pia alitembelea nchi jirani zinazopakana na taifa hilo la Pembe ya Afrika.

Hali katika Chad na Maziwa Makuu ilizingatiwa na Baraza la Usalama

Dimitri Titov, mkurugenzi wa kitengo kinachohusika na masuala ya Afrika cha Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani za UM (DPKO) majuzi alikuwa na mashauriano ya faragha na wajumbe wa Baraza, kuzingatia matokeo ya ukaguzi wa ziara ya ujumbe wa UM katika Chad kuhusu hali ya usalama, kwa ujumla, katika nchi.

Muda wa operesheni za UM katika DRC umeongezwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa operesheni za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika JKK (DRC), yaani MONUC, hadi mwisho wa mwaka. Huduma za ulinzi wa amani za MONUC zinatarajiwa kuimarisha vizuri zaidi hali ya utulivu katika eneo hili la Afrika ya Kati.

Sudan imekubali furushi la ulinzi wa amani kwa Darfur

Serekali ya Sudan wiki hii ilituma barua kwa Baraza la Usalama ilioelezea kukubali kupelekwa katika Darfur helikopta zitakazotumiwa na vikosi vya mseto vya AU na UM katika shughuli za kuimarisha usalama na amani kwa raia wa jimbo la magharibi la Sudan la Darfur.

Ajenda ya BU kwa Aprili itaongozwa na masuala ya Darfur na mabadiliko ya hali ya hewa

Balozi Emyr Jones Parry wa Uingereza aliwaambia wanahabari wa kimataifa kwenye Makao Makuu mjini New York, ya kwamba kutokana na muongezeko wa vurugu na hali ya wasiwasi katika jimbo la uhasama la Darfur, Sudan na athari zake kwa mataifa jirani, na pia tatizo la madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, Baraza la Usalama limeamua kuyapa masuala haya umuhimu zaidi katika mijadala yake ya Aprili.

Baraza la Usalama linazingatia masuala ya amani katika Afrika

Baraza la Usalama lilikutana kwenye kikao maalumu wiki hii kuzingatia ushirikiano kati ya mashirika ya kikanda na UM, hususan Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) kwa makusudio ya kuimarisha usalama na amani. Kikao kilitilia mkazo umuhimu wa kukuza ushirikiano huo na kuboresha uhusiano mwema kati ya UM na AU, kwa matarajio ya kuzuia ugomvi na mapigano yanayozuka mara kwa mara barani Afrika, na kusimamia kipamoja taratibu zinazotakikana kuleta suluhu ya kudumu ya migogoro husika.

Hapa na pale

Louise Arbour, Kamishna Mkuu juu ya Haki za Kibinadamu alifanya mahojiano wiki hii na wawakilishi wa vyombo vya habari waliopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UM) ambapo alionya kwamba licha ya kupatikana maendeleo karibuni katika ulinzi wa haki za kibinadamu, hususan katika mwaka huu - na kutoa mfano wa kupitishwa ule mkataba wa kupinga tabia ya kutorosha watu na kuwaangamiza - hata hivyo, yeye binafsi, alisema, anaamini bado mchango mkubwa ziada unahitajika katika sehemu nyengine za maamirisho ya haki za kibinadamu ulimwenguni, hususan katika juhudi za kukomesha kile alichokiita “msiba wa baa” la unyanyasaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake.~