Security Council

Ban atoa wito wa kutokuwepo na ghasia na kuheshimu haki za binadamu wakati maandamano yakiendelea Misri

Umoja wa Mataifa umeelezea hofu yake kuhusu hali inavyobadilika haraka nchini Misri.

Ban akutana na viongozi wa Cyprus wa upande wa Uturuki na Ugiriki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na viongozi wa Cyprus ya upande wa Uturuki na upande wa Ugiriki mjini Geneva.

Serikali ya mpito ya Somalia lazima imalize mwezi Augusti: Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga ametangaza kwamba mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Somalia utafanyika mjini Addis Ababa Ethiopia sambamba na ule wa muungano wa Afrika ulioanza leo.

Awamu ya mwisho ya mazunguzmo ya Sahara Magharibi yakamilika mjini New York

Awamu ya tano ya mazungumzo yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Sahara Magharibi yamekamilika huku Morocco na eneo la la Frente Polisario wakikubaliana kuendelea na mazungumzo hayo mwezi Machi.

Kupekuwa mgari ya UM Ivory Coast ni ukiukaji wa sheria

Umoja wa Mataifa umetoa onyo kwa uongozi wa Icory Coast kutosimamisha na kukagua magari ya Umoja wa Mataifa. Amri ya kufanya upekuzi ilitolewa kwa majeshi yanayomuunga mkono Rais Laurent Gbagbo kupitia vyombo vya habari vya serikali.

Baraza la usalama lapitisha kuongezwa vikosi vya UNOCI Ivory Coast

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limeidhinisha kuimarishwa mara moja vikosi vyake vya kulinda amani ivory coast vilivyo na wanajeshi karibu 9000 na kwa kuongezwa wengine 2000, na helkopta tatu za kijeshi kwa ajili ya kuwalinda raia kufuatia mvutano wa kisiasa wa baada ya uchaguzi.

Matokeo ya kura ya maoni Sudan yanakusanywa:Mkapa

Matokeo ya kura ya maoni ya kujitenga ama la kwa Sudan Kusini yanakusanywa pamoja hivi sasa kutoka vituo 3000 .

Mabadiliko kwenye baraza la usalama kuanza 2011:Deiss

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Joseph Deiss leo amesema ina matumaini kwamba mazungumzo hasa ya kupanua wigo wa baraza la usalama yanaweza kuanza mwaka huu.

Wafanyikazi wa WFP watekwa nyara Darfur Sudan

Wafanyakazi watatu wa ndege wanaofanya kazi na mpango wa Umoja wa Mataifa wa chakula duniani WFP wametekwa nyara kwenye jimbo la Darfur Sudan.

Baraza la usalama limealaani mashambulio dhidi ya UNOCI

Mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI yamelaaniwa na wajumbe wa baraza la usalama.