Security Council

Baraza la usalama limehitimisha ziara Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamehitimisha ziara yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

UM wajiandaa na kongamano wiki ijayo Uturuki kwa ajili ya kuisaidia Somalia

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Ahmedou Ould-Abdallah, amesema wakati wa kuchukua hatua kuinusuru Somalia ni sasa.

Baraza la usalama limejadili jinsi ya kuisaidia Nepal baada ya kuzuka mtafaruku

Baraza la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili kuhusu shughuli ya Umoja wa Mataifa katika kuisaidia jitihada za kupatikana kwa amani nchini NEPAL, baada ya makundi hasimu kukosa kuafikiana kuhusu maswala muhimu ya ugavi wa mamlaka na katiba mpya.

Volkano ya Iceland yachelewesha mpango wa makazi kwa wakimbizi wa Kipalestina

Kulipuka kwa volkani nchini Iceland wiki jana kumechelewesha mpango wa kuwapa makazi kundi la wakimbizi wa Kipalestina wanaotoka Iraq.

Japan inasema upokonyaji wa silaha za nyuklia lazima uwe na mtazamo maalumu

Wakati huohuo mwaka huu ni muhimu saana katika kuelekea kuwa na dunia isiyo na silaha za nyuklia, wakati ukijongea mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia na kuupitia mkataba wa kutozalisha nyuklia.

Mapendekezo ya vikwazo vipya kwa Iran yameanza kusambazwa

Mataifa muhimu ya magharibi na yenye nguvu yametuma mapendekezo ya vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa Urusi na Uchina. Vikwazo hivyo vitakilenga kikosi chenye nguvu nchini Iran cha wanamgambo wanamapinduzi, na kukaza uzi kwa vikwazo vilivyopo dhidi ya usafirishaji ,masuala ya bank na sekta ya bima.

Kikao cha 54 cha wanawake kimeanza New York

Leo kikao cha 54 cha wanawake kimeanza hapa mjini New York Marekani. Kikao hicho kinachohudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani na mashirika ya Umoja wa Mataifa, kitatathmini ajenda za mkutano wa Beijing uliofanyika mika 15 iliyopita.

Iran yatetea rekodi yake ya haki za binadamu

Jamuhuri ya Kiislamu ya watu wa Iran imetetea rekodi yake ya masuala ya haki za binadamu mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa. Inasema Iran ni sehemu ya vyombo vikubwa vya kimataifa vya haki za binadamu na imekuwa msitari wa mbele kutetea haki hozo.

Baraza la Usalama linaongeza muda wa vikosi vya UM nchini Cote d'Ivoire

Baraza la Usalama limeidhinisha Alhamisi, kuongeza muda wa afisi ya Umoja wa Mataifa nchini Cote d\'Ivoire, UNOCI pamoja na ule wa vikosi vya Ufaransa vinavowasaidia, kwa miezi minne zaidi ili kusaidia kuandaa uchaguzi wa huru, haki na wazi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mjumbe wa UM na Umoja wa Afrika amejadili Darfur na viongozi wa Sudan

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, Ibrahim Gambari, amekutana na waziri wa ulinzi wa Sudan kujadili mustakbal wa eneo la Darfur linalokumbwa na ghasia, kama sehemu ya mikutano kadhaa na viongozi wa Sudan .