Security Council

Mukhtasari wa shughuli za Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi lilikutana kwenye kikao cha hadhara, kuzungumzia ripoti inayohusu mradi wa viwanda vya nishati ya nyuklia katika Iran. Kadhalika, kwenye kikao cha faragha baadaye wajumbe wa Baraza la Usalama walishauriana juu ya fafanuzi za Kamati ya Vikwazo dhidi ya Sudan, pamoja na kusailia hali katika Myanmar na masuala mengineyo yenye kuhusu usalama na amani ya kimataifa.~

Baraza la Usalama lazingatia masuala ya Usomali na Cyprus

Baraza la Usalama, chini ya uraisi wa Balozi Michel Kafando wa Burkina Faso, linatarajiwa alasiri kuzingatia hali katika Usomali na suala la Cyprus.~

Ubelgiji itaongoza shughuli za BU kwa Agosti

Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Agosti ni Balozi Jan Grauls wa Ubelgiji ambaye hii leo baada ya mashauriano na wajumbe wa Baraza juu ya ajenda ya mwezi, anatazamiwa kuongoza majadiliano maalumu yatakayozingatia ripoti ya KM kuhusu hali katika Sierra Leone.

Mjumbe wa KM kwa Usomali ajasirisha BU kudumisha amani haraka katika Pembe ya Afrika

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali leo asubuhi alipohutubia mbele ya Baraza la Usalama juu ya hali katika Usomali aliwakumbusha wajumbe wa Baraza kuhusu wajibu walionao wa kuzingatia, kwa ujasiri mkubwa, uwezekano wa kubadili hadhi ya vikosi vya ulinzi wa amani vya UA vya AMISOM viliopo Usomali, ili vikosi hivyo vidhaminiwe madaraka mapya na viwe vikosi vya amani vya UM.

Hapa na Pale

Serge Brammertz Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya UM juu ya Makosa ya Vita kwa iliokuwa Yugoslavia (ICTR) amewasilisha ripoti maalumu kwa waandishi habari Ijumatatu (21 Julai) ya kupongeza kukamatwa kwa Radovan Karadzic, kiongozi wa kisiasa wa Waserb wa Bosnia na mtoro aliyekimbia adhabu ya sheria kwa muda mrefu katika Bosnia-Herzegovina. Karadzic alishikwa na wenye madaraka Serbia na sasa yupo kizuizini. Karadzic alishitakiwa rasmi na Mahakama ya ICTR miaka 13 iliopita kwa kuongoza makosa dhidi ya utu na mauaji ya halaiki kwa raia wa Bosnia-Herzegovina wasiokuwa Waserb - yaani Wacroat na WaIslamu wa huko. Tutakupatieni taarifa zaidi Ijumanne.

Hapa na Pale

Baraza la Usalama limekutana Ijumaa kuzingatai shughuli za Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) na pia kufanya mapitio ya ripoti ya KM kuhusu ombi la Nepal la kutaka UM usaidie kuimarisha mpango wa amani nchini humo. Baraza la Usalama limeamua kuongeza muda wa kazi kwa majaji wanaohusika na mauaji ya Rwanda, ili kuhakikisha kesi zilizosalia zinakamilishwa kwa muda unaotakiwa na ICTR.

Wapatanishi wa UM/UA kwa Darfur waripoti mbele ya BU juu ya hali ya amani kieneo

Wapatanishi wa UM na UA juu ya Darfur, yaani Jan Eliasson na Salim Ahmed Salim wamewasilisha ripoti zao mbele ya Baraza la Usalama kuhusu hali ya usalama na amani kwenye jimbo hili la mgogoro la Sudan magharibi. Mpatanishi wa UM Eliasson alisema kwenye risala yake kwamba yeye na Mpatanishi wa AU Salim wamependekeza kwa KM ateuliwe Mjumbe Maalumu juu ya Darfur, atakayekuwa na makao yake Khartoum, Sudan kushughulikia suala hilo, na wao wapo tayari kumsaidia mwakilishi huyo kwa kila njia kuleta amani kwenye jimbo la mgogoro.

Hali ya kisiasa Zimbabwe yapewa usikizi mkubwa na BU na KM

Alasiri Baraza la Usalama lilikutana, kwenye kikao cha hadhara/faragha, kujadilia hali halisi ya kisiasa nchini Zimbabwe kufuatia uamuzi wa Morgan Tsvangirai, wa chama cha upinzani cha MDC, kujitoa kugombania uchaguzi wa urais ambao unatarajiwa kufanyika nchini mwisho wa wiki. KM wa UM, Ban Ki-moon, katika risala yake kuhusu suala hili, alioitoa kwa kupitia Msemaji wake, alisema anakhofia kitendo cha kiongozi wa MDC kujitoa kwenye uchaguzi kinatia "wasiwasi wa kina" na hakiashirii mema kwa mfumo wa demokrasia katika Zimbabwe.

Mikutano ya Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi lilikutana kwenye kikao cha hadhara kusikiliza ripoti juu ya matokeo ya ziara ya karibuni ya tume ya Baraza ambayo ilitembelea Djibouti, Sudan, Chad, JKK na Cote d’Ivoire. Wawakilishi wa Kudumu wa Afrika Kusini na Uingereza walizungumzia kuhusu ziara ya ujumbe wa Baraza la Usalama katika Djibouti - kuzungumzia Usomali - na juu ya Sudan. Mjumbe wa Kudumu wa Ufaransa aliripoti kuhusu safari yao katika Chad na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo; na Balozi wa Burkina Faso, alityeipatia Baraza taarifa kuhusu Cote d\'Ivoire.

BU lasailia Zimbabwe kabla ya ziara ya Mjumbe wa KM

Baraza la Usalama (BU) leo limefanyisha kikao cha faragha kusailia tatizo la kiutu lilioselelea karibuni nchini Zimbabwe. Kikao hiki kinafanyika kabla ya KM Mdogo juu ya Masuala ya Kisiasa, Haile Menkerios hajaelekea Zimbabwe wiki ijayo, ambapo anatazamiwa kushauriana na viongozi husika kadha juu ya hali ya kisiasa, kwa ujumla, na vile vile kuzungumzia nawo kuhusu duru ya pili ya uchaguzi ujao wa uraisi utakaofanyika tarehe 27 Juni.