Security Council

UNHCR yahimiza mapigano yakomeshwe Kivu Kaskazini kunusuru raia

Antonio Gutteres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ambaye alizuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK)hivi karibuni, ametoa mwito wenye kuyanasihi makundi yote yalioshiriki kwenye uhasama na mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo, hali ambayo ikikamilishwa itayawezesha mashirika ya kimataifa yanayofadhilia misaada ya kiutu kupata fursa ya kuhudumia kihali umma muhitaji ulionaswa kwenye mazingira ya mapigano.

Baraza la Usalama laongeza madaraka ya shirika la BINUB Burundi

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa kazi za Ofisi ya UM inayosimamia ufufuaji wa shughuli za maendeleo katika Burundi (BINUB) hadi tarehe 31 Disemba 2008.

Baraza la Usalama kujadidisha vikwazo dhidi ya Liberia

Baraza la Usalama limepitisha azimio nambari 1792 ambalo limependekeza vikwazo vya silaha, na usafiri dhidi ya baadhi ya viongozi katika Liberia, viendelezwe kwa miezi 12 zaidi.

Ya hapa na pale

Miaka 15 baada ya kuanzishwa majadiliano ya kusailia taratibu za kuhifadhi misitu ya dunia na uharibifu, Baraza Kuu la UM limefanikiwa kupitisha azimio la khiyari litakalosaidia kuimarisha hifadhi bora ya hii rasilmali ya kimataifa.

Hali Usomali inawatia wasiwasi mkubwa wajumbe wa Baraza la Usalama

Baada ya mashauriano kukamilishwa ndani ya Baraza la Usalama juu ya hali katika Usomali, Balozi Marty Natalegawa wa Indonesia, Raisi wa Baraza kwa mwezi Novemba, aliwasilisha kwa waandishi habari taarifa ya pamoja, kwa niaba yawajumbe wa Baraza yenye kuelezea wasiwasi mkuu ulioivaa jamii ya kimataifa juu ya kuharibika kwa hali ya kisiasa, usalama na vile vile mazingira ya kiutu nchini Usomali.

Baraza la Usalama latoa mwito kwa Ethopia na Eritrea kutanzua mzozo wa mpakani

Baraza la Usalama limetoa mwito mapema wiki hii kuzihimiza Eritrea na Ethopia kutekeleza bila ya kuchelewesha uwamuzi wa 2002 juu ya mstari wa mpaka wao wa pamoja, likisisitiza haja ya mataifa hayo mawili jirani kutanzua matatizo yao kwa amani.

Baraza la Usalama laridhika na maendeleo ya utaratibu wa amani Uganda.

Baraza la Usalama la karibisha maendelo mazuri yaliyopatikana hivi karibuni katika utaratibu wa amani kati ya serekali ya Uganda na waasi wa Lord Resistance Army LRA, na kutoa mwito kwa pande zote mbili kutumia kila nafasi zilizo jitokeza kuendelea mbele na kuboresha maisha ya wakazi wa kaskazini ya Uganda.

Vikosi vya amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati

Baraza la Usalama limepitisha azimio muhimu lilioruhusu vikosi vya ulinzi wa amani vya UM na Umoja wa Ulaya kupelekwa katika Chad mashariki na sehemu za mashariki-kaskazini ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Vikosi hivi vinatazamiwa kuwapatia raia wa maeneo hayo hifadhi, na vile vile kuwapatia wahamiaji na umma uliong’olewa makwao ulinzi bora dhidi ya mashambulio ya kihorera.

Hapa na pale

KM amependekeza kwa Baraza la Usalama uteuzi wa kumfanya Ahmedou Ould Abdallah kuwa Mjumbe Maalumu mpya kwa Usomali, ofisa ambaye kwa sasa anaongoza Ofisi ya UM kwa Afrika Magharibi.~

Wajumbe wa Afrika Magharibi wamejadili tatizo la ugaidi

Zaidi ya darzeni moja ya nchi za Afrika magharibi zimekutana na mataifa fadhili na mashirika ya kimataifa wiki hii kujadili mahitaji ya kifundi katika kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi katika kana hiyo.