Security Council

Japan inasema upokonyaji wa silaha za nyuklia lazima uwe na mtazamo maalumu

Wakati huohuo mwaka huu ni muhimu saana katika kuelekea kuwa na dunia isiyo na silaha za nyuklia, wakati ukijongea mkutano wa kimataifa wa usalama wa nyuklia na kuupitia mkataba wa kutozalisha nyuklia.

Mapendekezo ya vikwazo vipya kwa Iran yameanza kusambazwa

Mataifa muhimu ya magharibi na yenye nguvu yametuma mapendekezo ya vikwazo vipya dhidi ya Iran kwa Urusi na Uchina. Vikwazo hivyo vitakilenga kikosi chenye nguvu nchini Iran cha wanamgambo wanamapinduzi, na kukaza uzi kwa vikwazo vilivyopo dhidi ya usafirishaji ,masuala ya bank na sekta ya bima.

Kikao cha 54 cha wanawake kimeanza New York

Leo kikao cha 54 cha wanawake kimeanza hapa mjini New York Marekani. Kikao hicho kinachohudhuriwa na maelfu ya wanawake kutoka sehemu mbalimbali duniani na mashirika ya Umoja wa Mataifa, kitatathmini ajenda za mkutano wa Beijing uliofanyika mika 15 iliyopita.