sayansi

Utafiti  na maendeleo kutatua changamoto za afya:WHO

Leo, Idara mpya ya sayansi ya shirika la afya ulimwenguni ,WHO imezindua rasilimali  muhimu mtandaoni ili kutoa muongozo wa kutengeneza  bidhaa mpya za afya ambazo zina masoko madogo au motisha kwa ajili ya utafiti na utengenezaji  wa bidhaa za tiba pamoja na maendeleo.

15 Mei 2019

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo assumpta Massoi anakuletea

-Mkutano wa sayansi na wabobevu wa ubunifu umekunja jamvi New york hii leo Dkt. Agness Kijazi kutoka Tanzania ni miongoni mwa washiriki utamsikia

Sauti -
12'23"

Nimedhamiria kudhihirisha kuwa sayansi si kwa wanaume tu- Fatima

Kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za utamaduni, takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa bado kuna umuhimu wa kuweka mazingira ya kuwahamasisha wasichana kujiunga katika fani za sayansi.

Sauti -
2'

Mchango wa wanawake na wasichana katika sayansi ni muhimu sana:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehimiza haja ya kuziba pengo la wanawake na wasichana lililopo katika nyanja ya sayansi, uhandizi na hisabati au STEM akisema mchango wao ni mkubwa na unahitajika.

Sauti -
1'21"

Wasichana wasiogope sayansi kwa sababu inatuzingira kila mahali- Bi Wahome

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi, Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN- Women na lile la  elimu sayansi na utamaduni, UNESCO yamesema sauti za wanawake na wasichana na ujuzi katika sayansi, teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuleta suluhu katika Dunia ya sasa ambayo inashuhudia mabadiliko ikiwemo mabadiliko haribifu.

11 Februari 2019

Katika Jarida la Habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

Sauti -
11'14"

Mchango wa wanawake na wasichana katika sayansi ni muhimu sana:Guterres

Ujuzi katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati unachagiza ubunifu na ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi.

Wanasayansi wasichana wa Afrika wako mstari wa mbele katika vita ya kuleta usawa wa kijinsia katika sayansi-Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hii mjini Addis Ababa Ethiopia amekutana na kuzungumza na wasichana kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambao wanashiriki katika mpango wa kuwafanya kubobea katika programu za kompyuta, mkakati wa unaoratibiwa kwa pamoja kati ya Muungano wa kimataifa wa Mawasilino (ITU) na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.