Sahel

Watu milioni 29 wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi ukanda wa Sahel 

Rekodi mpya ya juu inaonesha kuwa watu milioni 29 katika nchi sita yaani Burkina Faso, kaskazini mwa Cameroon, Chad, Mali, Niger na kaskazini mashariki mwa Nigeria - sasa wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi, hii ikiwa ni watu milioni tano zaidi ya mwaka jana.

Guterres alaani shambulio nchini Niger

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kikatili huko Niger ambalo limesababisha vifo vya watu 137.

Bado nina wasiwasi na hali ya inayoendelea Sahel:Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema licha ya maendeleo yaliyopatikana hivi karibuni katika mchakato wa amani na pia kufanyika kwa chaguzi kwa njia ya amani bado ana wasiwasi kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama Sahel hasa katika katika maeneo ya Liptako-Gourma ambako kuongezeka kwa machafuko kumefanya hali ya kibinadamu kuwa mbaya zaidi. 

Mizozo pembe ya Afrika na majanga ya asili Sahel yasukuma watu kuweka maisha yao rehani Mediteranea

Wakati zahma zikiongezeka katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara na kuwalazimisha mamilioni ya watu kufungasha virago, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi

Sauti -
2'36"

Chondechonde tuwanusuru wakimbizi na wahamiaji wanaolazimika kuvuka Mediterrania:UNHCR 

Wakati zahma zikiongezeka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na kuwalazimisha mamilioni ya watu kufungasha virago, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa raia ya kuongeza juhudi za kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji hasa wanaobidi kupitia njia hatari kwenye bahari ya Mediterrania kwenda kusaka mustakbali bora.

22 Januari 2021

Leo Ijumaa ni mada kwa kina ikijikita katika harakati za  ukuzaji wa lugha ya kiswahili nchini Tanzania na nje ya mipaka hiyo kupitia kufundisha lugha hiyo adhimu wageni bila kusahau umuhimu wa kujumuisha watu wenye ulemavu katika harakati hizo.

Sauti -
9'56"

Idadi ya wakimbizi wa ndani Sahel ni milioni 2, UNHCR yatoa wito kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi

Shirika la Umoja wa Matiafa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linatoa wito kusitishwa kwa ukatili unaoendelea katika ukanda wa Sahel ambao umesabaibsha watu takriban milioni mbili kuwa wakimbizi wa ndani. 

Mradi wa kuboresha mazingira Sahel GGW wapigwa jeki ya dola zaidi ya bilioni 14

Mradi kabambe wa kukabiliana na hali ya jangwa kwenye ukanda wa sahel na Sahara wa Great Green Wall, GGW  umepokea ufadhili wa dola bilioni 14.236 za kimarekani.