Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotolewa leo Ijumaa inasema mauaji, ubakaji na mifumo mingine ya ukatili inayowalenga jamii ya Wahema katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC inaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imeelezea wasiwasi wake juu ya msamaha wa rais wa Marekani kwa wanajeshi watatu wanaoshukiwa kutekeleza uhalifu wa kivita.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR , imeisihi serikali ya Zimbabwe isake njia bora ya kushughulikia machungu ya hali ngumu ya kiuchumi inayokumba wananchi badala ya kushambulia waandamanaji wanaolalama kuhusu mazingira duni.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR ina wasiwasi kuhusu taarifa kutoka Misri isemayo watu 15 wamenyongwa mwezi huu wa Februari ambapo watu tisa maisha yao yalikatiliwa isiku ya Jumatano wiki hii huku wengine sita walikabiliwa na hukumu ya kifo mapema mwezi huu.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imesikitishwa na vurugu za mashambulizi ya muda mrefu dhidi ya wapalestina ikirejelea shambulizi la hivi karibuni katika kijiji cha Al Mughayyir kilichoko katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan.
Wakati idadi ya watu waliouawa nchini Nicaragua tangu maandamano dhidi ya serikali yaanze nchini humo ikiwa ni takribani 280, Umoja wa Mataifa umesema ni dhahiri shahiri kuwa lazima ghasia hizo zikome hivi sasa.