UN yasema machafuko ya kikabila Ituri DRC yaweza kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotolewa leo Ijumaa inasema mauaji, ubakaji na mifumo mingine ya ukatili inayowalenga jamii ya Wahema katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC inaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.