Kura za maoni katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi haziwezi kuwa halali - UN
Msaidizi wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa na amani Rosemary DiCarlo amewaeleza Jumanne hii wajumbe wa Baraza la Usalama kuhusu kura ya maoni katika maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na majeshi ya Urusi; akidai kuwa upigaji kura haulingani na “udhihirisho wa kweli wa nia ya watu wengi.”