Uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe unakaribia na wito umetolewa leo kwa wadau wote serikali, vyama vya kisiasi na wafuasi wao kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika katika mazingira ya amani, utulivu , kuzingatia haki za binadamu na utawala wa sharia.
Shirika la fedha duniani, IMF limesema liko tayari kusaidia Zimbabwe kurejea ukuaji wake wa kiuchumi pamoja na utulivu kufuatia kuondoka madarakani kwa Rais Robert Mugabe.