Rendile

22 Juni 2018

Leo Ijumaa ya Juni 22 mwaka 2018, Assumpta Massoi anaangazia:

Sauti -
11'50"

Sisi ni warendile tutambulike tulivyo: Alice

Yaelezwa kuwa utamaduni ni kielelezo cha ustawi wa kila jamii. Utamaduni hudhihirishwa kwa njia mbalimbali iwe lugha, mila, mavazi, chakula na kadha wa kadha. Kutotambulika kwa utamaduni wa mtu au jamii ina maana ni kutokomea kwa jamii hiyo na ndio maana jamii ya warendile walioko kaunti ya Marsbit nchini Kenya wanapaza sauti ili kabili hilo litambuliwe kwa kina ili hata mila zao basi ambazo si potofu ziweze kutumiwa katika kusongesha maisha si tu kwenye jamii zao bali pia kwingineko ambako zinafaa. 

Sauti -
3'48"

22 Machi, 2018

Katika Jarida hii leo, Siraj Kalyango anaangazia siku ya Maji tukimulika wakazi wa jamii ya warendile huko Marsabit nchini Kenya. Vijana wakutana New York, Marekani kujifunza muundo wa UN. Sudan Kusini wakimbizi wa ndani waanza kurejea wakimwomba mola awageukie.

Sauti -
10'20"

Maji safi bado mkwamo kwa warendile huko Marsabit

Leo ni siku ya maji duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo uhifadhi wa mazingira halisi ya eneo husika kama njia moja ya kukabiliana na uhaba wa maji duniani.

Sauti -
1'31"

Maji safi bado mkwamo kwa waRendile huko Marsabit

Leo ni siku ya maji duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo uhifadhi wa mazingira halisi ya eneo husika kama njia moja ya kukabiliana na uhaba wa maji duniani.

15 Machi 2018

Jaridani leo tunaangazia maswala ya haki za kibinadamu kwa wakimbizi wa Palestina faida ya kuinua wanawake vjijini. Pia tunakuletea makala ikiangazia vikwazo vya umiliki ardhi miongoni mwa wanawake Tanzania. 

Sauti -
11'41"

Faida ya kuinuliwa nawe uinuwe wengingine:KPL

Kikao cha 62 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kikiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani, washiriki wanaendelea kupigia chepuo juhudi za ukombozi wa wanawake na wasicha wa vijijini kwa kuelezea wanachokifanya. Leo tumekutana na mwanaharakati kutoka nchini Kenya.