Washindi wa tuzo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018 hii leo wamepatiwa tuzo hizo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani.
Leo washindi wa tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa akiwemo Rebeca Gyumi kutoka Tanzania wanakabidhiwa tuzo hizo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjini New York Marekani.
Rebeca Gyumi, mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana nchini Tanzania pamoja na watu wengine wawili na shirika moja la kiraia, wameshinda tuzo ya mwaka huu ya haki za binadamu