Rasimu ya azimio la Marekani dhidi ya Hamas yagonga mwamba Baraza Kuu
Rasimu ya azimio lililowasilishwa na Marekani dhidi ya kundi la Hamas kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imegonga mwamba hii leo baada ya kutopata kura za kutosha kutoka kwa wajumbe. Rasimu hiyo iliyojadiliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani ni ya kulikosoa kundi la Hamas kwa kuvurumisha maroketi hadi Israel kutokea Ukanda wa Gaza.