Wasichana shirikini michezo kwa kucheza na kutangaza
Radio, michezo na jinsia ni mada ambayo imechambuliwa kwa kina na vijana wa mtandao wa wanahabari vijana kutoka Mwanza nchini Tanzania. Uchambuzi huo umeendana na maudhui ya siku ya redio duniani hii leo ya Radio na Michezo. Katika makala hii, mwanahabari kijana Rashid Malekela anazungumza na vijana wenzake wa kike na wa kiume kufahamu ni kwa jinsi gani mada hizo zinaoana na zaidi ya hapo zinasaidiaje kubeba jukumu kubwa la radio la kuliemisha, kuhabarisha na kuburudisha.