Radio

29 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

Sauti -
11'40"

Redio bado ni chombo chenye nguvu-Antonio Guterres

Jumatano hii, kama ilivyo ada kila mwaka Februari 13, dunia inaadhimisha siku ya redio duniani ujumbe ukiwa majadiliano, uvumilivu na amani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kwa ulimwengu kuhusu siku hii amesema redio ni chombo chenye nguvu. 

Kijana mkimbizi atumia radio chakavu kurusha matangazo huko kambini Kyangwali nchini Uganda

Leo Ijumaa katika makala kwa kina tuko nchini Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali, ambako John Safari, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ametumia ubunifu na ujuzi wa kukarabati redio na kuanzisha mtambo wa kurusha matangazo ya  redio yanachohabarisha jamii ya wakim

Sauti -
5'12"

TV bado haijapoteza dira licha ya teknolojia mpya:UN

Televisheni bado ni chombo muhimu cha mawasiliano duniani licha ya kuzuka kwa teknolojia mpya ambazo zimechukua nafasi kubwa ya maisha ya watu, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni, UNESCO. 

Kipindi cha radio kutumika kuelimisha jamii kuhusu uhamiaji holela nchini Nigeria

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa,  IOM limezindua kipindi cha Radio nchini na Nigeria kiitwacho Abroad Mata kwa lengo la kuelimisha  umma kuhusu madhara  ya uhamiaji holela na fursa za kuhama kwa kufuata kanuni.

Japo haiwasahaulishi madhila Radio yawahabarisha wakimbizi wa Rohingya

Mawasiliano ya radio ni muhimu sana kwa jamii yoyote, kwani mbali ya kuburudisha pia huelimisha na kufikisha tarifa muhimu kwa jamii husika, vivyohivyo kwa wakimbizi wa Rohingya walio kambini kwenye makazi ya Katupalong nchini Bangladesh. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mawasiliano ni muhimu sana hasa jamii kama ya Rohingya wanaoishi kambini. 

Rumbek 98 FM mnachohitaji sasa ni jua tu kusikika hewani kila siku- UNMISS

Wananchi wa Rumbek nchini Sudan Kusini, sasa watahabarika kutwa nzima kila siku, tena kwa kupitia lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya mama Dinka, Kiarabu na Kiingereza baada ya Radio pekee ya jamii inayoendeshwa na serikali ya Rumbek 98FM kupigwa jeki na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS. 

Radio haitokufa, na inaendelea kuwa na umuhimu mkubwa: IOM

Baadhi ya watu wamekuwa wakidai Radio ni chombo cha habari kinachokufa , lakini ukweli ni kwamba Radio imezidi kushamiri na itaendelea kuwa chombo muhimu cha mawasiliano katika jamii ndani na nje ya masuala ya kibinadamu.

Utangazaji michezo redioni umeniimarisha- Jane John

Utangazaji wa michezo kupitia redio umenisaidia siyo tu kutambulika bali pia kujifunza mengi na hivyo kuimarisha stadi zangu na kuhabarisha jamii inayonisikiliza.

Sauti -
1'17"

Utangazaji michezo redioni umeniimarisha- Jane John

Utangazaji wa michezo kupitia redio umenisaidia siyo tu kutambulika bali pia kujifunza mengi na hivyo kuimarisha stadi zangu na kuhabarisha jamii inayonisikiliza.