Ushirikiano baina ya nchi za Asia ya Kati na Afghanistan ni dhahiri- Guterres
Umoja wa Mataifa umesema uko tayari kusaidia nchi za Asia ya Kati zinapoimarisha ushirikiano baina yao na Afghanistan ili kufanikisha malengo ya amani, maendeleo endelevu, utulivu na usalama.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema hayo leo wakati akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama uliokutana kujadili ubia wa kikanda kati ya Afghanistan na Asia ya Kati.
Bwana Guterres ametolea mfano ushirikiano wa kielimu uliopo sasa kati ya Kazakhstan na Afghanistan..
(Sauti ya António Guterres)