Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer, amesema hakuna mtu yeyote atakayefurushwa kwenye vituo vya ulinzi wa raia, POC, vilivyofungua milango yake wakati ghasia zilipozuka nchini humo mwaka 2013 kunusuru raia waliokuwa wanasaka maeneo salama.