Plastic

Ukikusanya chupa kulinda mazingira utazawadiwa:Inuka Foundation

Chupa na hasa la plastiki imekuwa moja ya tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira duniani na juhudi zinafanyika katika ngazi mbalimbali kuhakikisha taka hizo haziendeleo kuzagaa au kuishia baharini.

Sauti -
4'

Mjasiriamali ageuza taka kuwa vifaa vya ujenzi nchini kenya

Lengo nambari 13 la malengo ya maendeleo endelevu SDG’s au ajenda ya 2030, linahimiza  Umoja wa Mataifa ya mashirika yake kuweka msisitizo katika utekelezaji wa ulinzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na utokomezaji wa matumizi ya bidhaa za plastiki.

Sauti -
5'53"

Dau lilitengenezwa kwa mabaki ya taka za plastiki litasafiri kati ya miji mikongwe ya Afrika Mashariki.

Dau la kijadi lililotengenezwa na taka za plastiki zilizookotwa pwani ya Kenya na miji mbalimbali litaanza safari yake ya kwanza tarehe 24 mwezi huu kutoka mji mkongwe wa Lamu nchini Kenya hadi mji mkongwe huko Zanzibar nchini Tanzania tarehe 7 mwezi ujao, ikiwa ni safari ya umbali wa kilometa 500.