Vyombo vya habari tangazeni habari zinazoinua wanawake-Phumzile
Umoja wa Mataifa umetaka vyombo vya habari nchini Tanzania kupazia sauti habari ambazo zinamnyanyua mwanamke kama njia mojawapo ya kujenga uwezo wa watoto wa Kike na wanawake wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN-WOmen, Phumzile Mlambo-Ngucka amesema hiyo jijini Dar es salaam, kando mwa mkutano kuhusu jinsia na masuala ya habari.