Katibu Mkuu atuma rambirambi kwa familia na watu wa Oman kufuatia kifo cha Sultan Qaboos
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya kifalme, serikali na watu wa Oman kufuati kifo cha Sultan Qaboos Said ambaye alifariki usiku wa Ijumaa akiwa na umri wa miaka 79.