ohchr

Mtaalamu huru asitisha ziara yake Comoro

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji, Nils Melzer, amesitisha ziara yake aliyokuwa afanye Comoro, baada ya kukumbwa na vizuizi vya hapa na pale.

Mashambulizi dhidi ya raia nchini Mali yakome- Mtaalamu

Mashambulizi yanayoendelea kila uchao nchini Mali dhidi ya raia yanaweza kuwa uhalifu dhidi ya binadamu na hivyo ni lazima hatua zichukuliwe kulinda raia na mali zao.

Hali ya utesaji binadamu na ukiukwaji wa haki Comoro kuangaziwa

Masuala ya ukiukwaji wa haki za binadamu hususan watu kuteswa kinyume cha kanuni nchini Comoro yatamulikwa na kufanyiwa tathmini wakati wa ziara ya wiki moja ya mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji, Nils Melzer.

Kiendeleacho Sudan tunataka kichunguzwe- OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imependekeza kupelekwa haraka timu ya Umoja wa Mataifa ya waangalizi wa haki za binadamu nchini Sudan ili kufuatilia madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika tangu Juni 3 mwaka huu 2019. Grace Kaneiya na taarifa kamili.

Sauti -
1'35"

Timu ya haki za binadamu ipelekwe Sudan kufuatilia kinachoendelea:OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imependekeza kupelekwa haraka timu ya Umoja wa Mataifa ya waangalizi wa haki za binadamu nchini Sudan ili kufuatilia madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika tangu Juni 3 mwaka huu 2019.

Nchi za Ulaya zatakiwa kusitisha kupeleka dizeli chafu Afrika

Kuelekea siku ya mazingira duniani hapo kesho Juni 5 ambayo inaangazia shughuli mbalimbali za binadamu zinasochafua hali ya hewa, mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu taka hatarishi na za sumu ameonya kampuni za Ulaya ambazo zinauzia nchi za Afrika nishati chafuzi ikiwem

Sauti -
2'4"

Nchi za Ulaya acheni kupeleka dizeli chafu na yenye sumu Afrika- Mtaalamu

Kuelekea siku ya mazingira duniani hapo kesho Juni 5 ambayo inaangazia shughuli mbalimbali za binadamu zinasochafua hali ya hewa, mtaalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu taka hatarishi na za sumu ameonya kampuni za Ulaya ambazo zinauzia nchi za Afrika nishati chafuzi ikiwemo mafuta ya dizeli yenye kemikali za sumu. 

UN yalaani mauaji na kushikiliwa kwa waandamanji wakati wa maandamano ya amani Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amelaani vikali ukatili na ripoti za matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia nchini Sudan, vitendo ambavyo vimeripotiwa kusababisha vifo na majeruhi.

Kamishna Mkuu Bachelet ataka uchunugzi kuhusu kifo cha Hassan Toufic Dika wa Lebanon

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ametaka kufanyike uchunguzi wa kina na ulio huru, kuhusu kifo cha mfungwa mwenye miaka 44 - mwanamume raia wa Lebanon Hassan Toufic Dika, kilichotokea tarehe 11 mwezi huu.

Kushikilia na kuua watu bila sababu Myanmar ni kinyume cha sheria:UN

Kukamatwa kwa vijana na wanaume wanaokadiriwa kuwa 40 hadi 50 nchini Myarmar ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa dhidi ya mustakabali wao imesema ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa hii leo.