Wataalamu 7 wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka Misri ilinde uhuru wa wananchi kujieleza, kukusanyika kwa amani na kujiunga kwenye vikundi wakati huu ambapo taifa hilo limeshuhudia mlolongo wa matukio ya kukamatwa kwa waandamanaji, wanahabari na watetezi wa haki za binadamu nchini humo.