Ikiwa zimebakia siku 9 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet ameelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya ghasia zilizoripotiwa katika majimbo matatu nchinu humo wiki hii wakati wa kampeni za uchaguzi.