Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Ocean

UNDP/Pierre Michel Jean

Ripoti ya FAO yaonesha mchango wa uvuvi na ufugaji wa samaki katika kuimarisha uhakika wa upatikanaji wa chakula

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiwa katika siku ya tatu hii leo huko Lisbon nchini Ureno Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ongezeko kubwa la ufugaji wa samaki sambamba na uvuvi wa kimataifa umesababisha mazao ya vyakula vya majini kuwa kwenye rekodi ya juu katika kuchangia kwa kiasi uhakika wa chakula na lishe katika karne hii ya Ishirini na moja.

Taarifa ya Leah Mushi.

Sauti
2'26"
Unsplash/Shane Stagner

Mvuvi aliyegeukia kilimo cha Mwani aeleza alivyonufaika

Moja ya malengo ya Mkutano wa bahari unaoendelea Lisbon, Ureno, ni kujadili namna ambavyo dunia inaweza kuendelea kunufaika kiuchumi kutokana na uwepo wa bahari. Ajenda hiyo inakuwa muhimu kwa kuwa tayari ni dhahiri shairi kuwa baharí imekuwa mkombozi wa kiuchumi kwa watu wengi duniani. Mfano wa wazi ni Amiri Juma Amiri, mkazi wa kijiji cha Kibuyuni katika Kaunti ya Kwale huko Pwani ya Kenya, mkulima wa zao la mwani ambalo hulimwa baharini.

Taarifa ya Anold Kayanda. 

"Mimi katika hii kazi ya mwani nilikuwa siifanyi.Nilikuwa ninafanya kazi ya uvuvi."

Sauti
2'58"
Amiri Juma Amiri mkulima huyu wa mwani akiwa na mwani aliovuna kutoka shambani kwake baharini kufuatia mradi unaofadhiliwa na taasisi ya utafiti wa majini na viumbe vya  bahari ya Kenya.
UN/ Kenya

Kilimo cha mwani baharini kimenitoa kwenye nyumba ya tope – Amiri wa Kibuyuni, Kwale - Kenya

Moja ya malengo ya Mkutano wa bahari unaoendelea Lisbon, Ureno, ni kujadili namna ambavyo dunia inaweza kuendelea kunufaika kiuchumi kutokana na uwepo wa bahari. Ajenda hiyo inakuwa muhimu kwa kuwa tayari ni dhahiri baharí imekuwa mkombozi wa kiuchumi kwa watu wengi duniani. Mfano wa wazi ni Amiri Juma Amiri, mkazi wa kijiji cha Kibuyuni katika Kaunti ya Kwale huko Pwani ya Kenya, mkulima wa zao la mwani ambalo hulimwa baharini.

Sauti
2'58"