Chuja:

Nuhu Zuberi Bakari

UN News Kiswahili

Neno la wiki - Bumbuwazi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia neno "Bumbuwazi". Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA . 

Bwana Nuhu anasema unapopigwa na butwaa ama kupatwa na mshangao, hadi ukawa huwezi kuongea hata neno moja basi utakuwa umepigwa na bumbuwazi.

Sauti
13"

Neno la Wiki- Mhanga, Manusura na Muathirika

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Mhanga”, "Manusura" na “Muathirika”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo..

Sauti
58"

Neno la wiki: Mhanga, Manusura na Muathirika

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Mhanga", “Manusura” na "Muathirika".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo..

Neno la Wiki: tofauti za Supu na Mwengo ni zipi?

Wiki hii tunaangazia maneneno "Supu” na “Mwengo" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema sio kila kitu ambacho kimepikwa katika maji ni Supu. Mwengo ni aina ya supu itokanayo na kupika viumbe vya bahari kwa maji, kama vile samaki, pweza, ngisi. Ukitaka kuagiza supu yake unasema naomba mwengo wa samaki, mwengo wa pweza au mwengo ya ngisi…

Sauti
48"

Neno la Wiki: Halisi, Uhalisi, Uhalisia

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Halisi", “Uhalisi” na "Uhalisia".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo, ambayo hutumiwa ndivyo sivyo…

Sauti
1'11"

Neno la Wiki: Halisi, Uhalisi, Uhalisia

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno “Halisi”, "Uhalisi" na “Uhalisia”.  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Ungana naye upate matumizi sahihi ya maneno hayo, ambayo hutumiwa ndivyo sivyo...

Neno la wiki: Zuzu na Bwege

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno "Zuzu" na "Bwege".  Mchambuzi wetu  ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Nuhu anasema zuzu ni mtu ambaye hana akili timamu, mtu ambaye akifunzwa hata hafunziki. Zuzu pia unaweza kumwita mjinga, zezeta au mpumbavu. Bwana Bakari akaenda mbali zaidi kuchambua neno bwege akisema halina tofauti sana na zuzu, kwa maana kwamba ni mtu nduguye. Mathalani bwege ni mtu ambaye amekaa kizoleazolea au mbumbumbu.