Walinda amani wa Tanzania nchini DRC watunukiwa nishani za Umoja wa Mataifa
Walinda amani kutoka Tanzania, Kikosi cha 8 cha kujibu mashambulizi kinachohudumu katika ulinzi wa amani chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, FIB MONUSCO wametunukiwa nishani ya Umoja wa Mataifa katika sherehe zilizopambwa kwa gwaride maalum lililoandaliwa na kikosi hicho. Afisa habari wa TANZBATT8, Kapteni Tumaini Bigambo alikuwepo katika hafla hiyo ana ametuandalia ripoti ifuatayo.