Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia maadhimisho ya miaka 75 tangu bomu la atomiki lilipodondoshwa katika mji wa Nagasaki, Japan, amewasifu hibakusha, yaani waathirika wa shambulio hilo la bomu la nyuklia, ambao wamegeuza shida yao ya miongo kadhaa kuwa onyo juu ya hatari ya silaha za nyuklia na katika mfano wa ushindi wa roho ya mwanadamu.